Ubaguzi wa rangi Marekani hautaisha – LeBron James

Mchezo wa mpira wa vikapu kwenye league ya NBA, LeBron James amesema suala la ubaguzi wa rangi haliwezi kuisha katika nchi ya Marekani dhidi ya watu weusi.

LeBron amezungumza hayo siku ya jana kufuatia kuchorwa neno *Nigga* na watu waiojulikana katika ukuta wa nyumba yake ya Los Angeles. Neno hilo linaashiria tusi kwa mtu mweusi, amesema LeBron tokea mji wa San Francisco, ambako timu yake imeweka kambi ya mazoezi kabla mchezo wa 1 wa fainali za NBA.

“Hata uwe na pesa kiasi gani , hata uwe na umaarufu kiasi gani ,kuwa mtu mweusi nchini Marekani ni vigumu ,”Ubaguzi wa rangi siku zote utakuwa sehemu ya dunia, sehemu ya Marekani, na chuki nchini Marekani ,hasa kwa waMarekani wenye asili ya Afrika na upo kila siku ,tuna safari ndefu kama jamii, hasa sisi kama waMarekani wenye asili ya Afrika hadi tutakapohisi tuko na usawa Marekani” alisema LeBron .

LeBron James mwenye umri wa miaka 32 anatambuliwa kama mchezaji anayelipwa zaidi katika ligi ya NBA, kwa kulipwa kitita cha zaidi ya dola milioni 20 kwa mwaka. Nyota huyo tokea NBA alitangazwa kuwa ndio mchezaji aliyefunga vikapu vingi katika mchezo wa kikapu nchini Marekani ,na kufanikiwa kuvunja rekodi ya nguli wa mchezo huo, Michael Jordan.
Previous
Next Post »