Waimbaji
wa Kundi la Bongofleva la Navy Kenzo ambalo limepata mafanikio kimuziki Aika na Nahrel wametoa maoni yao kuhusu wimbo mpya wa Ben Pol pamoja na tukio lake la kupiga
kisha kupost kwenye Instagram picha akiwa bila nguo na kupakwa mafuta.
Aika na Nahrel wamefunguka kupitia XXL ya Clouds FM leo June 2, 2017
wakisema wimbo mpya wa Ben Pol unaoitwa
Tatu ni mbaya na hauendani na namna alivyopiga picha na kupakwa mafuta:>>>“Unajua Tanzania tuna utamaduni
wetu. Nadhani hata Baraka maoni yake siyo kashfa lakini ni maoni yake. Tuna
utamaduni binafsi tunachukulia vitu kibinadamu lakini nadhani maoni
yanaruhusiwa.” – Nahrel.
“Ulichokisema na sisi tulikiongea vivyo hivyo.
Nahrel baada ya kuona Baraka the Prince ametuma ile comment kwenye Group
tulisema kwamba wasanii wote kama wangekuwa na uwezo kama wa Baraka the Prince
kuongea kile wanachojisikia moyoni, basi nafikiria tungeenda mbali sana maana
wengi sana wanakuwa wandanganyana (Siyo mimi lakini nimesema kuwa nyimbo
mbaya)”. – Aika.
EmoticonEmoticon