Watu 36 wauawa mjini Manila, Ufilipino


Watu 36 wamefariki dunia na wengine takriban 50 wamejeruhiwa katika jumba la kuchezea la kamari la Resorts World Manila lililopo mjini Manila, Ufilipino.

Mtu mmoja aliyekuwa na silaha ambaye alinaswa na kamera za CCTV zilizokuwa katika eneo hilo, alifyatua risasi mfululizo katika jumba hilo pamoja na kuwasha moto ambao ulisababisha watu wengi kufariki kutokana na kukosa hewa safi.

Hata hivyo maafisa wa polisi katika mji huo wamesema baada ya mtu huyo kutekeleza tukio hilo na yeye mwenyewe alijiuwa.

Taarifa ambayo imetolewa na polisi hao imesema kuwa mtu huyo ambaye hakufahamika jina lake anaonekana alikuwa na matatizo ya akili.
Previous
Next Post »

EmoticonEmoticon

:)
:(
=(
^_^
:D
=D
=)D
|o|
@@,
;)
:-bd
:-d
:p
:ng